
Evans aondolewa kwenye kikosi cha Ireland
Beki wa Leicester City, Jonny Evans atakosa mechi ya ufunguzi ya kufuzu michuano ya Euro kwa kikosi cha Ireland Kaskazini dhidi ya San Marino na Finland.
Evans mwenye umri wa miaka 35 ameondolewa kwenye kikosi kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya misuli yanayomsumbua.
Siku ya Alhamisi kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers amesema kuwa beki huyo wa kati anasumbuliwa na majeruhi ambayo yalianza toka mwezi Novemba.
Baada ya kutolewa kwenye mechi ya Novemba 8 mwaka jana mchezaji huyo aliingia kama mchezaji wa akiba kwenye mechi ambayo walifungwa 3-1 dhidi ya Chelsea.
Kikosi cha Michael O'Neill kitaanza kampeni ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Euro ambapo watacheza na San Marino siku ya Alhamisi na siku ya Jumapili watacheza dhidi ya Finland.